Machapisho

Katiba kwenye mtazamo wa miraba tatu (Sehemu II-I): Kugeuza katiba bila Kura ya maoni

Picha
Istilahi ‘Kura ya Maamuzi’ sasa imeanza kutumika ni kama ni sawia na kugeuza katiba. Katika mijadala nyingi zinazohuzisha akina yakhe, na nyakati zingine hata wataalam; kuna mwegemeo unaolenga kuashiria kuwa hakuna jinsi ingine ya kurekebisha katiba (kwa juhudi pana) bila kupiga kura hiyo. Imesemwa na kubalika kuwa asilimia 20 ya katiba ina kasoro, ila hakujakuwa na makubaliano ya ni nini ndio kasoro mahususi inayozungumziwa. Kila mtathmini ana maoni yake tofauti. Hiyo basi, huenda kupata uwiano dhabiti kwenye swala hili utachukua muda mrefu sana. Hati hii ya katiba ilikosa kizungu cha kutosha. Imebahatisha matumizi ya istilahi Marekebisho kumaanisha geuzo lolote katika katiba. Ilhali, katiba ya Marekani hutumia neno hilo kumaanisha kuboresha au kuimarisha hoja ama sheria, hapa Kenya tumewai kulitumia kumaanisha geuzo lolote bila kujali athari epuka. Hivo basi, katiba ya 1963 ilifanyiwa Marekebisho mengi ingawa yakiwa ya ubomofu na kudunisha sheria. Basi, itafaa Su