Machapisho

Katiba kwenye mtazamo wa miraba tatu (Sehemu II-I): Kugeuza katiba bila Kura ya maoni

Picha
Istilahi ‘Kura ya Maamuzi’ sasa imeanza kutumika ni kama ni sawia na kugeuza katiba. Katika mijadala nyingi zinazohuzisha akina yakhe, na nyakati zingine hata wataalam; kuna mwegemeo unaolenga kuashiria kuwa hakuna jinsi ingine ya kurekebisha katiba (kwa juhudi pana) bila kupiga kura hiyo. Imesemwa na kubalika kuwa asilimia 20 ya katiba ina kasoro, ila hakujakuwa na makubaliano ya ni nini ndio kasoro mahususi inayozungumziwa. Kila mtathmini ana maoni yake tofauti. Hiyo basi, huenda kupata uwiano dhabiti kwenye swala hili utachukua muda mrefu sana. Hati hii ya katiba ilikosa kizungu cha kutosha. Imebahatisha matumizi ya istilahi Marekebisho kumaanisha geuzo lolote katika katiba. Ilhali, katiba ya Marekani hutumia neno hilo kumaanisha kuboresha au kuimarisha hoja ama sheria, hapa Kenya tumewai kulitumia kumaanisha geuzo lolote bila kujali athari epuka. Hivo basi, katiba ya 1963 ilifanyiwa Marekebisho mengi ingawa yakiwa ya ubomofu na kudunisha sheria. Basi, itafaa Su...

Jinsi mawaziri wa fedha walivyodhibiti viwango vya riba na akiba

Picha
Kiwango cha riba na akiba za mabenki ni chombo muhimu sana kwa kukuza biashara na uchumi. Hii ni kwa sababu viwango viliopo huchangia kuvutia ama kutimua wateja ambao mara nyingi huwa ni wafanyibiashara. Kiwango cha kukopa kikiwa juu, wakopi hushindwa kulipa madeni yao. Lakini, wakopeshaji   wakiwa na mioyo ya kibepari kama Shailoki wa Venisi, hukimbilia   kuuza mali yao bila huruma wakidai walipwe kwa ‘haki na haka ya hati yao’. Kenya, kama nchi, imelaumiwa   kwa kuwa na kiasi kidogo cha uwekezaji wa   akiba. Hata hivyo, wakosoaji   wamekataa kutambua kuwa faida ya mtu kuziacha pesa benki ni duni. Hii ni kufuatia   kuwa mvuvumko wa bei ya bidhaa mara nyingi huwa juu kushinda mapato yanaolipwa na hazina za benki   au taasisi zingine za kifedha. Hali hii huwatoa watu hamu ya kuwaacha pesa kwa akaunti   ya hazina. Lakini juhudi za serikali zinawezadhibiti tabia mbaya ya taasisi za fedha na mabenki kama picha hapo...