Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2013

Shilingi kwa ya pili; mbona hazishabihiani?

Picha
Ninaomba maafisa   wa Benki Kuu au Hazina Kuu   ya kitaifa wajibike na kutueleza sisi Wakenya kinagaubaga, ni sarafu ipi ya shilingi yetu ndio halisi? Ni bayana kwamba sarafu ni kigezo muhimu cha dhamani   ya mali. Hivyo basi, kigezo hicho inafaa kiwe   ama kifanywe dhabiti. Ni mara ngapi maafisa kutoka idara ya vipimo na ubora huwashambulia wenye maduka wanaotumia ratili   ambazo hazina usawa na ulinganifu wa wastani uliyowekwa? Si mawe ya ratili zote yamepewa uzito sawia ili kuhakikisha kwamba viwango vinatoshelezwa?  Itafaa zaidi kama tutatumia sarafu moja ya kutegemewa na wala tusipewe shiligi moja ya fedha iliyo kubwa, ingine ya fedha iliyo ndogo na hata isitoshe moja ya shaba iliyo ndogo kushinda hata senti kumi! Na tuambiwe kuwa shilingi ni shilingi   bora tu iwe na mhuri wa Benki Kuu  Ni ukweli noti zetu zinatosheleza ubora wa ulinganifu wa kimuondo ila, duniani kote inajulikana kuwa ni pesa za sarafu ndizo zenye kuamika zaidi kwa maana zinawakilisha dhamani y