FALSAFA
Falsafa ni nini? Falsafa ni juhudi ya kuuliza, kufahamu na kujibu maswali sugu kwa tafakuri. FALSAFA YA KIAFRIKA NA YA ULAYA FALSAFA YA KIAFRIKA Inaweza kugawanywa katika sehemu zifuatazo mbili. Yani, falsafa ya Kiafrika ni aidha Kiujumla: Falsafa yoyote ile ambayo itaguzia maudhui ya kiafrika au itatumia mbinu za kiafrika kukidhi madhumuni yake. Kimaalum: Falsafa ile tu imetokana na mtu ambaye ni Mwafrika au an uzao wa Kiafrika. Falsafa ya Kiafrika inachukua daraja tatu 1. Uhenga-tamaduni: Weledi wa mambo yote ya mila ya watu wa jamii fulani. Hapa kuna Falsafa-tamaduni: Weledi wa mila na desturi za jamii na unamilikiwa na watu wote wa jamii hiyo ila, wazee ni wahenga zaidi kuliko watoto. Falfasa-uhenga: Weledi wa mambo ya mila na tamaduni za jamii zilizomo kwenye mhenga mmoja mashauri. Falsafa-shehe: Mweledi wa mambo ya mila na tamaduni za jamii pamoja na mambo mengi ya malimwengu 2. Falsafa-itikadi: Uanzilishi ama uzinduzi wa mfumo wa fikira wa ku