Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2017

Jinsi mawaziri wa fedha walivyodhibiti viwango vya riba na akiba

Picha
Kiwango cha riba na akiba za mabenki ni chombo muhimu sana kwa kukuza biashara na uchumi. Hii ni kwa sababu viwango viliopo huchangia kuvutia ama kutimua wateja ambao mara nyingi huwa ni wafanyibiashara. Kiwango cha kukopa kikiwa juu, wakopi hushindwa kulipa madeni yao. Lakini, wakopeshaji   wakiwa na mioyo ya kibepari kama Shailoki wa Venisi, hukimbilia   kuuza mali yao bila huruma wakidai walipwe kwa ‘haki na haka ya hati yao’. Kenya, kama nchi, imelaumiwa   kwa kuwa na kiasi kidogo cha uwekezaji wa   akiba. Hata hivyo, wakosoaji   wamekataa kutambua kuwa faida ya mtu kuziacha pesa benki ni duni. Hii ni kufuatia   kuwa mvuvumko wa bei ya bidhaa mara nyingi huwa juu kushinda mapato yanaolipwa na hazina za benki   au taasisi zingine za kifedha. Hali hii huwatoa watu hamu ya kuwaacha pesa kwa akaunti   ya hazina. Lakini juhudi za serikali zinawezadhibiti tabia mbaya ya taasisi za fedha na mabenki kama picha hapo juu inavyoonesha. Ni bayana kuwa siku