Shilingi kwa ya pili; mbona hazishabihiani?
Ninaomba maafisa wa Benki
Kuu au Hazina Kuu ya kitaifa wajibike na
kutueleza sisi Wakenya kinagaubaga, ni sarafu ipi ya shilingi yetu ndio halisi?
Ni bayana kwamba sarafu ni kigezo muhimu cha dhamani ya mali. Hivyo basi, kigezo hicho inafaa kiwe ama kifanywe dhabiti. Ni mara ngapi maafisa
kutoka idara ya vipimo na ubora huwashambulia wenye maduka wanaotumia ratili ambazo hazina usawa na ulinganifu wa wastani uliyowekwa?
Si mawe ya ratili zote yamepewa uzito sawia ili kuhakikisha kwamba viwango
vinatoshelezwa?
Itafaa zaidi kama tutatumia sarafu moja ya kutegemewa na
wala tusipewe shiligi moja ya fedha iliyo kubwa, ingine ya fedha iliyo ndogo na
hata isitoshe moja ya shaba iliyo ndogo kushinda hata senti kumi! Na tuambiwe
kuwa shilingi ni shilingi bora tu iwe na
mhuri wa Benki Kuu
Ni ukweli noti zetu zinatosheleza ubora wa ulinganifu wa kimuondo
ila, duniani kote inajulikana kuwa ni pesa za sarafu ndizo zenye kuamika zaidi
kwa maana zinawakilisha dhamani ya madini yaliomo na sio tu mhuri wa benki. Basi ni heri wataalamu husika waanze kulinganisha
sarufi za pesa zetu ili tuwe na moja tu ambayo ni wastani kutuelekeza kutathmini bei halisi ya bidhaa zilizoko sokoni, gharama
ya maisha na dhamani ya pesa za kigeni.
Edwin Musonye
Maoni
Chapisha Maoni