Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2017

Jinsi magavana wa Benki Kuu wamekabiliana na mvuvumiko wa bei tangu Kenya kupata Uhuru

Picha
Tangu tupate Uhuru wa nchi mwaka wa 1963, tumekuwa na magavana 9 wa benki kuu. Magavana hawa bila shaka walijitahidi na kukabiliana na mfuriko wa bei kama ilivyo jukumu lao. Lakini ni bayana kuwa wengine hawakutia bidi ipasavyo, na hivyo, hawakudhibiti hali ngumu ya maisha kwa wananchi. Hata hivyo sote tunafahamu kuwa mbinu walionazo wakati mwingine si tosha kutimiza lengo hilo. Ndio basi tunawakashifu waliolemewa kwa huruma.  Hata hivyo, pia gavana mkaidi ama baramaki anawezavuruga uchumi kwa   kuweka sera duni za kifedha kama vile kuuidhinisha kuchapishwa sarafu zaidi kuliko kiwango hitajika. Utepetevu   mwingine unatokana na kukoza kukagua mabenki za biashara vyema. Gavana mwangaifu anafahamu kuwa jukumu lake ni kutetea sera za kukuza uchumi ya nchi na si kuwafurahisha wanasiasa. Ni vyema basi kumpa kondele bw. Micah Cheserem kwa kuweka rekodi   ya gavana aliyeshukisha mvuvumiko wa bei kwa kiwango cha juu zaidi kutoka kwa mtangulizi wake.

Ukuaji wa uchumi wa Kenya

Picha
Ukuaji wa uchumi wa Kenya pasi kupanda kwa gharama ya maisha 1964 -2010. Taarifa : Kumbukumbu za serikali | Document Point