Jinsi mawaziri wa fedha walivyodhibiti viwango vya riba na akiba
Kiwango cha riba na akiba za mabenki ni chombo muhimu sana kwa kukuza
biashara na uchumi. Hii ni kwa sababu viwango viliopo huchangia kuvutia ama
kutimua wateja ambao mara nyingi huwa ni wafanyibiashara. Kiwango cha kukopa
kikiwa juu, wakopi hushindwa kulipa madeni yao. Lakini, wakopeshaji wakiwa na mioyo ya kibepari kama Shailoki wa Venisi,
hukimbilia kuuza mali yao bila huruma
wakidai walipwe kwa ‘haki na haka ya hati yao’.
Kenya, kama nchi, imelaumiwa kwa
kuwa na kiasi kidogo cha uwekezaji wa akiba. Hata hivyo, wakosoaji wamekataa kutambua kuwa faida ya mtu kuziacha
pesa benki ni duni. Hii ni kufuatia kuwa
mvuvumko wa bei ya bidhaa mara nyingi huwa juu kushinda mapato yanaolipwa na hazina
za benki au taasisi zingine za kifedha. Hali
hii huwatoa watu hamu ya kuwaacha pesa kwa akaunti ya hazina.
Lakini juhudi za serikali zinawezadhibiti tabia mbaya ya taasisi za fedha
na mabenki kama picha hapo juu inavyoonesha. Ni bayana kuwa siku za zamani
kidogo, viwango za riba viikuwa vimedhibitiwa na hivyo vilikuwa na adabu.
Nyakati za James Gichuru, Mwai Kibaki na Arthur Magugu kama mawaziri wa fedha
(1963-1988) upenu kati ya kiwango cha kuwekeza na cha kukopa kilikuwa chini -yani
si zaidi ya mara dufu.
Ila , wazimu ulingia (1988-1992) wakati George Saitoti alikuwa kwenye
usukani. Kwa bahati nzuri Musalia Mudavadi alipongia, alifanya juhudi kupindua
mtindo na kiwango cha kukopesha kikaanza kushuka. Mtindo huo uliendelea hadi David Mwiraria na Uhuru
Kenyatta walipolegea kazini. Lakini, kwa bahati nzuri tena, Robinson Githae
alikaidi mtindo huo mapema kwenye mwaka wa (2011) na mambo yameebakia shwari hadi leo.
Hivyo basi, sheria ya kudhibiti viwango vya riba ni sharti iendelee
kuungwa mkono hata kama wakopeshaji wamehodhi
pesa na kukataa kupeana mikopo wakidai eti watapata hasara. Nia na mbinu
zao mbovu za biashara ziendelee kukashifiwa wa wote nchini.
Maoni
Chapisha Maoni