Jinsi magavana wa Benki Kuu wamekabiliana na mvuvumiko wa bei tangu Kenya kupata Uhuru
Tangu tupate Uhuru wa nchi mwaka wa 1963, tumekuwa na
magavana 9 wa benki kuu. Magavana hawa bila shaka walijitahidi na kukabiliana
na mfuriko wa bei kama ilivyo jukumu lao.
Lakini ni bayana kuwa wengine hawakutia bidi ipasavyo, na
hivyo, hawakudhibiti hali ngumu ya maisha kwa wananchi. Hata hivyo sote
tunafahamu kuwa mbinu walionazo wakati mwingine si tosha kutimiza lengo hilo.
Ndio basi tunawakashifu waliolemewa kwa huruma.
Hata hivyo, pia gavana mkaidi ama baramaki anawezavuruga
uchumi kwa kuweka sera duni za kifedha
kama vile kuuidhinisha kuchapishwa sarafu zaidi kuliko kiwango hitajika.
Utepetevu mwingine unatokana na kukoza
kukagua mabenki za biashara vyema.
Gavana mwangaifu anafahamu kuwa jukumu lake ni kutetea sera
za kukuza uchumi ya nchi na si kuwafurahisha wanasiasa. Ni vyema basi kumpa
kondele bw. Micah Cheserem kwa kuweka rekodi
ya gavana aliyeshukisha mvuvumiko wa bei kwa kiwango cha juu zaidi
kutoka kwa mtangulizi wake.
Maoni
Chapisha Maoni