IKTISADI
Iktisadi ni nini?
Iktisadi ni sayansi ya kijamii inayo husika
na jinsi matarajio na mahitaji mengi ya jamii yanawezatoshelezwa na raslimali
haba.
Wanaiktisadi ni wanasayansi na kwa hivyo
wanawezakutoa kauli mbili: kauli thabiti na kauli ya kimapendekezo.
Kauli thabiti: Hizi ni kauli zinazowezadhibitishwa
kwa kufanyiwa utafiti, kwa mfano: bei zikishuka, bidhaa zitanunuliwa kwa wingi
zaidi.
Kauli pendekezi: Haya ni mapendekezo tu,
kwa mfano: Serikali inafaa ipunguze ushuru kwa bidhaa muhimu. Hivyo basi,
wanaiktisadi mara nyingi hawaakifikiani.
KUUNDA MODELI/NATHARIA
1. Jumlisha dhana
2. Tunga miongozo
3. Dhibitisha miongozo
4. Matokeo yakitoshana na = ukweli wa mambo
5. Basi inakuwa natharia
Modeli husaidia kurahisisha kuelezea dhana tofauti
tofauti. Katika somo la kiuchumi, modeli/natharia huchukua mfano ya chati.
Raslimali za kiuchumi:
Pia zinawezaitwa Viungo vya Kuzalisha Uchumi navyo ni
1. Ardhi – Raslimali yote halisi iliyopo
pahali fulani.
2. Leba–Bidii ya kutumia misuli na akili
3. Mtaji – Uwekezaji wa mali zote zisizo
halisi.
4. Tarazaki –Bidii ya kujumlisha viungo hizo
tatu ili kuzalisha bidhaa na huduma.
MATAWI YA IKTISADI
1. Iktisadi
Finyu: Inashugulika na maswala ya kambuni ama sekta ya
2. Iktisadi Pana:
Inashughulika na uchumi wa nchi, fedha na biashara ya kimataifa
MIFUMO ZA KIUCHUMI
Mfumo wa kiuchumi ni jinsi uchumi umeundwa na
kuenezwa. (Pia jinsi maswali nyeti yanavyo jibiwa).
Hukuna hali kama mfumo pangwa kamilifu au
huru kamilifu. Nchi zote zimechanganya hali hizi mbili kwa kiasi fulani.
Kuna, kwa msingi, aina tatu za mifumo za kiuchumi
duniani nazo ni
1. Pangwa (Ujamaa)
2. Huru (Ubinafsi)
3. Mchanganyiko
Tofauti kati ya mahitaji na mapambo
MAHITAJI:
Hizi ni bidhaa muhimu katika maisha ya
binadamu. Na zinajumlisha chakula, makao na mavazi.
MAPAMBO:
Hizi ni bidhaa ambazo zinaongeza starehe
katika maisha ya wanadamu nazo zinajumlisha televisheni, rununu, gari n.k.
UHABA
Uhaba ndio shida kuu ya kiuchumi. Hakuna
wakati ambapo mtu, jamii kambuni ama nchi itakuwa na raslimali nyingi hata
ikakosa haja ya kuitunza.
Ni uhaba huu unaofanya jamii zote kuboresha
njia za kufanya uamuzi baina ya mapendekezo yaliopo.
MASWALI MAALUM YANAYO WAKABILI WANAUCHUMI
1. Nini kizalishwe?
2. Kwa kiwango kipi?
3. Kizalishwe vipi?
4. Kizalishwe wakati gani?
5. Kuzalishia nani?
6. Kuzalishia wapi?
Kila chaguo ina hasara yake. Katika somo la
iktisadi hasara inayoletwa kwa kutupilia mbali pendekezo ilikuchagua pendekezo
ingine ni hasara ya hitari.
HASARA YA HITARI: Ni ile kupotea kwa faida
ingalililetwa na pendekezo iliyotupiliwa mbali.
Hata hivyo wanauchumi huonelea kuwa watu
hutumia busara kila wanapofanya maamuzi kwa hivyo pendekezo linalochaguliwa
huwa ni lile lenye kuleta faida kubwa kushinda lile ambalo halikuchaguliwa.
Tofauti kati ya mfumo pangwa na mfumo huru
Mfumo huru
1. Raia wanamiliki viungo vya uzalishaji
2. Faida ndio dhamira ya uzalishaji
3. Mteja ndio mfalme
4. Soko linaamua bei
5. Kuna ushindani sokoni
6. kupunguza hasara ni muhimu
Mfumo pangwa
1. Serikali inamiliki viungu vya usalishaji
2. Kutosheleza umma ndio dhamira ya
uzalishaji
3. Serikali ndio mfalme
4. Serekali inamua bei
5. Hakuna ushindani sokoni
6. Usawazishaji ni muhimu
Ubora wa mfumo huru
·
Bidhaa za hali ya juu
·
Uchumi unapanuka haraka
·
Maendeleo ni mengi
·
Raslimali inatumika kikamilifu
·
Aina nyingi za bidhaa sokoni
·
Watu wengi wanaridhishwa
Upungufu wa mfumo huru
·
Pengo kubwa baina matajiri na maskini
·
Bidhaa ni za hali ya chini
·
Bidhaa hatari zinawezauzwa
·
Mazingira yanaharibiwa
·
Ushindani unaweza kuwa mkali
kupindukia
·
Bei ya bidhaa inapaa
·
Sehemu zingine zinastawi zaidi
kuliko zingine
Ubora wa mfumo pangwa
·
Inapunguza pengo kati ya
matajiri na fukara
·
Bidhaa duni hazizalishwi
·
Mazingira haiharibiwi
·
Ajira zinahifadhiwa
·
Bei zinadhibitiwa
Upungufu wa mfumo pangwa
·
Uchumi inalimatia
·
Maendeleo ni machache
·
Bidhaa ni za aina kidogo
·
Watu hawatoshelezwi kikamilifu
·
Ubunifu uko chini
MWAFAKA
WA BEI
Katika soko huru mivuto ya hamu ya kununua
na hamu ya kuuza ndio huamua bei ya bidhaa
HAMU (GHASHI) YA KUNUNUA: Ni hamu ya
mnunuzi kutaka kununua bidhaa au huduma ikiwa imewekewa bei fulani.
HAMU (DHATI) YA KUNUNUA: Ni madhumuni ya mnunuzi
kununua bidhaa au huduma kiasi fulani kwa bei maalum.
Mambo yanayodhuru (ghashi) hamu ya kununua
·
Ubora k.v. rangi, uzito, nguvu n.k
·
Hitari na kuthamini ya
kibinafsi
·
Matangazo ya kibiashara
·
Uwepo wa bidhaa hiyo sokoni
·
Idadi ya watu
·
Sera za serekali
·
Mahali
·
Mapato ya mnunuzi
Mambo yanayodhuru (dhati) hamu ya kununua
Ni moja tu nayo ni BEI (yake) na bei ya bidhaa
badala au bidhaa ambatani)
KAULI YA HAMU YA KUNUNUA
Mambo yote yakisalia sare, bei ya bidhaa
ikipanda, hamu dhati ya kununua bidhaa hiyo itashuka. Yani kuna uhusiano kinzani
baina ya bei na kiasi cha bidhaa.
HAMU (GHASHI) YA KUUZA: Ni hamu ya muuzaji
kutaka kuuza bidhaa au huduma ikiwa imewekewa bei fulani.
HAMU (DHATI) YA KUUZA: Ni madhumuni ya
muuzaji kutaka kuuza bidhaa au huduma kiasi fulani kwa bei maalum.
Mambo yanayodhuru hamu (ghashi) ya kuuza
·
Gharama ya uzalishaji
·
Sera za serekali (ushuru ama
usaidizi)
·
Uwepo wa raslimali
·
Hali ya anga
·
Idadi ya wazalishaji
·
Teknolojia
·
Matarajio ya msalishaji
·
Wepesi wa kuifadhi bidhaa.
Mambo yanayodhuru hamu (dhati) ya kuuza
Ni moja tu nayo ni BEI ya bidhaa
KAULI YA HAMU YA KUUZA: Mambo yote
yakisalia sare, bei ya bidhaa ikipanda, hamu dhati ya kuuza bidhaa hiyo
itapanda. Yani kuna uhusiano sambamba baina ya bei na kiasi cha bidhaa.
Maoni
Chapisha Maoni