Katiba kwenye mtazamo wa miraba tatu (Sehemu II-I): Kugeuza katiba bila Kura ya maoni




Istilahi ‘Kura ya Maamuzi’ sasa imeanza kutumika ni kama ni sawia na kugeuza katiba. Katika mijadala nyingi zinazohuzisha akina yakhe, na nyakati zingine hata wataalam; kuna mwegemeo unaolenga kuashiria kuwa hakuna jinsi ingine ya kurekebisha katiba (kwa juhudi pana) bila kupiga kura hiyo.

Imesemwa na kubalika kuwa asilimia 20 ya katiba ina kasoro, ila hakujakuwa na makubaliano ya ni nini ndio kasoro mahususi inayozungumziwa. Kila mtathmini ana maoni yake tofauti. Hiyo basi, huenda kupata uwiano dhabiti kwenye swala hili utachukua muda mrefu sana.

Hati hii ya katiba ilikosa kizungu cha kutosha. Imebahatisha matumizi ya istilahi Marekebisho kumaanisha geuzo lolote katika katiba. Ilhali, katiba ya Marekani hutumia neno hilo kumaanisha kuboresha au kuimarisha hoja ama sheria, hapa Kenya tumewai kulitumia kumaanisha geuzo lolote bila kujali athari epuka. Hivo basi, katiba ya 1963 ilifanyiwa Marekebisho mengi ingawa yakiwa ya ubomofu na kudunisha sheria. Basi, itafaa Sura ya 16 yenye kichwa: MAREKEBISHO YA KATIBA HII itoe ufafanuzi wa neno hilo Marekebisho ili tusirejelee makosa ya hapo nyuma.

Isitoshe, waadishi aidha walipungukiwa kwa utaalam wa uandishi wa hati za aina hii, au walikosa ujuzi wa mawasiliano ya kiufundi. Hati hiyo imewasilshwa kwa mfumo wa ripoti na pendekezo zaidi kuliko mfumo wa mwelekezo. Upungufu huu unadhihirika tena kwenye sharia ya Kambuni na pia zenye kuunda mashirika mengi ya umma.

Kuzuia uwezekano wa kurudishwa nyuma katika hatua zilizopigwa, inawezakuwa heri kutofautisha ngazi za ubadilishaji wa hati kwa kuleta msamiati mpya kama ifuavyo,


Kubadilisha: Utunzi wa hati mpya ambayo ina mkusanyiko wa uhariri, usahihishi, urekebishi, na/ ama ustawishi yenye nia ya kupindua kabisa hati hiyo.

Kustawisha: Hiyo pachiko ambayo inastawisha ama kuboresha manuio yaliyomo kwenye Hati ya Haki; ama kupendekeza haki ingine mpya.

Kurekebisha: Ile kuongeza, kuhamisha, au kutoa afisi ya uakilishaji / jukumu; au hadhi ya afisi / maafisa.

Kusahihisha: Ile kuongeza, kuhamisha, au kutoa afisi huru / / jukumu; au  hadhi ya afisi / maafisa

Kuhariri: Kugeuza maneno, vishanzi, vifungu, sehemu ya hati iliyopo iliongeza usanifu na/ama ufasaha. Ila, uhariri hautakiwi kugeuza maana ya awali.

Kugeuza: Yote hapo juu


Kifungu 255 (1) (a) – (j) [ya sura 16] kimearidhisha ‘hoja 10 nyeti ‘ ambazo lazima kura ya maoni iamue kugeuzwa kwao. Ilihali, hoja hizo 10 zilitundikwa pamoja mbelini labda kwa ukosefu wa muda, ni vyema   sasa, kurejelea na kukagua na kupanga hoja hizo kwa makundi maalum kama ifuatavyo, 



Swala

Mchakato

Toleo

Jinsi geuko linavyodhihirika

Mkusanyiko wa  haririsho, sahihisho, rekebisho, na/au stawisho ambayo ina nuia kupindua kabisa hati iliyopo.

Kubadilisha
Badilisho
Nje ya hati; na kupindua hati ya awali.

Hati mpya inachukua mwaka wa uzinduzi k.m. Katiba 1963, 2010 n.k.

Hati ya Haki
c)  mamlaka ya watu
e)  Hati ya Haki
(a) mamlaka  ya Katiba
(b) mipaka ya Kenya

Kustawisha
Stawisho
Kama pachiko  na kujumlishwa kwa tarakimu k.m. 1, 2, 3 n.k.
 Uakilishi
(f) kipindi cha urais
h) majukumu ya Bunge
(i) malengo, kanuni na muundo wa serikali ya ugatuzi

Kurekebisha
Rekebisho
Ndani ya hati; na kupindua 
Sehemu, *kishanzi, kipengee, au sura ya awali.

Afisi huru; Maadili ya kitaifa, Kanuni za kiutawala
(g) uhuru wa Idara ya Mahakama, Tume, na afisi huru zinazorejelewa katika Sura ya Kumi na tano
(d) maadili ya kitaifa, kanuni za kiutawala zilizoorodheshwa katika Kifungu cha 10(2) (a) hadi (d)

Kusahihisha
 Sahihisho
Ndani ya hati; na kupindua  
Sehemu, *kishanzi, au sura ya awali.



Kurejelea/ Rudufu/ Pangilia

(j) mwelekezo wa Sura 16

Kuhariri
Haririsho
Ndani ya hati; na kupindua maandishi (neno, *kishanzi, kifungu, sentensi) ama akifisho ya awali.

Baadhi/au yote hapo juu

Kugeuza
Geuzo
Kama ilivyo *thaminiwa kwa kila kumbo


Tunavyo endelea kukuwa kidemokrasia na mifumo ya uongozi,  ni sharti tuendelee kubuni mbinu na kuongeza maarifaa ili tuweze kulinda maendeleo ipasavyo.  Ikiwa ni kweli kuwa asilia 80 ya katiba ni nzuri, basi lazima megeuzo yoyote mapya yasidhulumu wema huo.  

Isipokuwa ‘hoja 10 nyeti ‘ katika Kifungu 255 (1) (a) – (j), katiba inaweza kugeuzwa bila kura ya maamuzi kama ilivyosawiriwa hapa juu.



Edwin Musonye & Patrick Musindi
Mawasiliano ya Kiufundi, kambuni ya Document Point

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FALSAFA

IKTISADI